Wabunge Kutoka Vyama vya Upinzani Nchini wamesusia kuhudhuria kuapishwa kwa wabunge saba wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane wa Bunge la 11 ulioanza leo kwa madai hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho.
Katika mkutano huo ulioanza leo Mjini Dodoma na moja ya mambo yaliyopangwa kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa wabunge wapya 8 wa Viti Maalumu ambao wameteuliwa kuziba nafasi za wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofukuzwa uanachama wa chama hicho.
Aidha, Wabunge ambao wamekula kiapo cha uaminifu leo Septemba 5 ni pamoja na Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.
-
Lema apigwa marufuku kufanya mkutano
-
Lissu apingwa, atakiwa kutoigeuza TLS kama taasisi yake binafsi
-
Zitto: Uhuru wa demokrasia unaminywa nchini
Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa uapisho wa Wabunge hao wa CUF, wabunge wa upinzani waliingia bunge huku Spika Job Ndugai, akiwapiga kijembe cha kuhoji kwanini walikuwa wamevaa nguo nyeuzi wote.