Mashabiki wa Mbeya City wamekuwa kero kwa wachezaji wa Simba SC kuelekea mchezo wao wa kesho wa ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Asubuhi ya leo kundi la wanachama na mashabiki wa klabu hiyo lilivamia mazoezi ya Simba na kujaribu kuzuia wasifanye mazoezi katika uwanja wa Sokoine wakidai kuwa leo ilikuwa ni zamu yao kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Taarifa zilizoifikia tovuti hii zimesema kuwa wakati wachezaji wa Simba wakiwasili uwanja wa Sokoine wanachama na wapenzi wa Mbeya City ambayo nayo imekuwa timu ya wanachama yenye matawi mengi jijini Mbeya waliibuka ghafla uwanjani hapo na kudai kuwa Simba haikustahili kufanya mazoezi leo katika uwanja huo na kwamba timu yao ya Mbeya City ndio ambayo ilistahili kuutumia uwanja huo maandalizi ya mchezo wa kesho.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ni kwamba timu mgeni anatakiwa kuutumia uwanja utakao tumika kwa mchezo ujao ili kuzoea mazingira ya kiwanja husika kabla ya mchezo.

Habari zaidi zinasema hizo zilikuwa ni mbinu na kero za kawaida za mashabiki wa Mbeya City kuelekea kwa wachezaji wa Simba ambazo zimekuwa zikijitokeza tangu msimu wa kwanza timu hiyo ilipopanda daraja.

Chanzo cha habari kwa Dar24 kimekaririwa kikisema “tunawashangaa mashabiki wa Mbeya City kujaribu kutengeneza upinzani kwa Simba kila msimu tangu walipopanda daraja, unajua hii si mara yao ya kwanza kutufanyia ujinga huu sio kwamba hawajui kanuni wanafanya makusudi”

“Simba ni timu kubwa imeshazoea vitu kama hivi si Tanzania tu hata nje ya nchi kwetu sisi hili jambo dogo ndio maana hatukushughulika nao kwani wanajua kanuni inasema nini”

Simba inakutana na Mbeya City kesho ikiwa na kumbukumbua ya kufungwa mara mbili msimu uliopita wakifungwa 2-1 mzunguko wa kwanza uwanja wa taifa kabla ya kukutana na kisago kingine cha 2-0 uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

 

Tanzia: Deo Filikunjombe, Capt. W Silaa Wafariki Kwa ajali Ya Chopa
Utafiti Wabaini Tabia Hizi Kwa Watu Wenye ‘Tattoo’ Mwilini