Wachezaji wa ligi ya Marekani ya ‘NFL’ waligoma kusimama wakati wimbo wa taifa wa Marekani ulipokuwa ukipigwa katika uwanja wa Wembley ikiwa ni inshara ya kuonyesha Umoja wa kupinga sera za Donald Trump dhidi ya wanamichezo.
Tukio hilo limetokea wakati wa mchezo baina ya timu za Baltimore Ravens na Jacksonville Jaguars za marekani ikiwa ni siku chache baada ya rais Donald Trump kutaka wachezaji wanaokaidi kuheshimu wimbo wa taifa kufukuzwa kazi.
Wakati wimbo wa taifa ukipigwa baadhi ya wachezaji walisimama huku wakiwa wamekunja mikono ya na wengine walipiga magoti kitu ambacho hakiruhusiwi wakati wa wimbo wa taifa.
-
Lebron James amtusi Trump
-
PSG yashindwa kutamba bila Neymar
-
Mwambusi akana kutaka kurejea Mbeya City
Hapa chini video inayoonyesha hali ilivyokuwa wakati wimbo wa taifa ukipigwa;
Baada ya tukio hilo Trump ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa tweeter kulaani walichokifanya wachezaji kukaidi kuheshimu wimbo wa taifa.
Baadhi ya wanamichezo wamekuwa wakionyesha hisia zao juu kutopenda sera za Trump na Shahid Khan ambaye ni kiongozi wa Timu ya JacksonVille Jaguars aliungana na wachezaji kupinga yanayofanywa na Rais Trump.