Mcheza kikapu wa Marekani Lebron James amemtukana rais wa Marekani Donald Trump kwa kumuita ‘Bum'(Makalio) kufuatia matamshi ambayo Trump aliyotoa kuhusu mchezaji mwenzake Steph Curry.

Mabingwa wa ligi ya kikapu ya NBA ambao ni Golden State Warriors walialikwa Ikulu ya Marekani kusherekea ubingwa wao lakini mchezaji nyota wa timu hiyo Stephen Curry hakutaka kwenda Ikulu hivyo rais Trump kuandika katika ukurasa wake wa Tweeter kuwa mualiko huo umefutwa.

Baada ya Trump kutoa matamshi hayo Lebron James mwenye umri wa miaka 32 alijibu kwa kusema ”Kwenda Ikulu ya Whitehouse ilikuwa heshima lakini sio heshima tangu ulipoingia wewe”

Kwa upande Stephen Curry Curry alisema kuwa kukataa kwa timu yake kwenda Ikulu timu hiyo kunaweza kushinikiza mabadiliko katika ikulu hiyo kwani kuna vitu ambavyo Trump amekuwa akifanya visivyowapendeza wamarekani.

Steph Curry na Le Bron James

”Sitaki kwenda Ikulu kwa sababu itaonyesha kuwa wachezaji hawajui vitu ambavyo amekuwa akisema na vitu ambavyo hakusema kwa nia nzuri”, alisema Curry.

 

 

PSG yashindwa kutamba bila Neymar
Sita washambuliwa kwa tindikali