Jumla ya wahamiaji  1796  wamefukuzwa nchini  Tanzania na idara ya uhamiaji baada ya kungundua wageni hao hawana uhalali wa kuishi nchini na wameingia kinyume cha taratibu na sheria

Akizungumza leo na waandishi wa habari kaimu kamishna utawala na fedha na msemaji mkuu wa idara ya uhamiaji TanzaniaBw. Abbas Irovya amesema kuwa takwimu za januari mpaka aprili zinaonesha Tanzaniaimepokea wageni 4792.

DSC_1063

Hata hivyo amesema kuwa kwa sasa wananchi wamekuwa na uelewa hivyo baadhi hutoa ushirikiano pale waonapo watu wasiowajua katika maeneo yao” lakini hata hivyo bado elimu inahitajika zaidi kwa wananchi”

Aidha katika zoezi maalumu la kuwaondoa wahamiaji haramu Bw. Irovya amesisitiza waajiri wote kila ifikapo  robo ya mwaka wanapaswa kutoa taarifa juu ya wageni wanao waajiri na kutokufanyahivo ni kukiuka sheria ya 1995 namba 07 ya idara ya uhamiaji.

Amefafanua kuwa  Tanzania ni nchi inayozungukwa na majirani wengi sana na kwamba imepakana na nchi 8 kwa karibu  na kudai kuwa ni lazima sheria zifuatwe waingiapo wageni.

Pamoja na hayo kati ya wageni 4792 wageni 1417 kesi zao bado zipo mahakamani, waliofungwa ni 132 kwa kukutwa na hatia, kesi 509 upelelezi unaendelea, na kesi 383 zinaendlea katika mahakama mbalimbali nchini na wageni walioachwa huru ni 904.

 

Lema: Sishangai Waziri kuingia Bungeni Amelewa wakati kulikuwa na bar ndani ya uzio wa bunge
Majaliwa:Mataifa yaliyoendelea yashirikiane na Serikali ya Tanzania kuwahudumia wakimbizi