Siku moja baada ya mtandao wa Football Leaks kuanika hadharani mkataba wa mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya FC Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior, waingereza wameanza kumkebehi kwa kumfananisha na wachezaji wanaocheza katika ligi ya nchini England.

Neymar ambaye alidhaniwa analipwa mshahara mkubwa kama ilivyo kwa akina Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo, amefananishwa na mchezaji kama Jonjo Shelvey anayecheza nafasi ya kiungo kwenye klabu ya Newcastle Utd.

Gazeti la Telegraph mapema hii leo, limetoka na taarifa inayoesema kwamba, Njonjo Shelvey ni bora kuliko Naymar ambaye anacheza kwenye klabu inayowania ubingwa wa barani Ulaya.

Muandishi wa habari hiyo amefafanua kwamba, Njonjo anaonekana kuwa bora dhidi ya Neymar kutokana na mshahara wake kuwa juu ya mshambuliaji huyo kutoka nchini Brazil ambaye jana ilionekana analipwa kiasi cha Pauni elfu sabini na saba (77,000) kwa juma.

Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Telegraph, imeonekana kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 analipwa mshahara wa Pauni elfu themanini (80,000), na hapo ndipo muandishi alipotumia ujasiri wa kumkebehi Neymar kupitia mshahara wake wa kila juma.

Njonjo amekuwa katika mikakati ya kukisaidia kikosi cha Newcastle Utd kupambana na kushuka daraja kutokana na chombo chao kwenda mrama katika msimamo wa ligi ya nchini England, lakini kwa upande wa Neymar hali inaonekana kuwa shwari akiwa na FC Barcelona.

Jambo linguine lililompa ujasuiri muandishi wa habari hiyo, ni hatua ya kuuzwa kwa Njonjo kutoka Swansea kuelekea Newcastle Utd mwanzoni mwa mwaka huu, huku akiwa hana sifa ya kufunga bao hata moja kwa msimu huu, ikifananishwa na Neymar ambaye kwa wastani wa kawaida ndani ya mwezi hufunga zaidi ya mabao mawili.

Mshangao uliopo unagonga vichwa vya mashabiki wa soka duniani kwa kuhoji iweje anaepigania klabu yake isishuke daraja analipwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko yule ambaye amesaidiana na wengine kuiweka FC Barcelona mahala penye usalama wa hali ya juu zaidi.

West Ham Utd Wadhamiria Kumrejesha Carrick Jijini London
Real Madrid Kuziingiza Vitani Chelsea Na Manchester United