Mwanariadha wa Kenya Ezekiel Kemboi ameshinda medali ya nne mfululizo katika mashindano ya dunia ya riadha yanayoendelea mjini Bejjing nchini China, baada ya kuwashinda wakenya wenzake.

Awali mwanariadha wa Kenya Vivian Ceruiyot aliiwezesha nchi yake kutwaa medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 10,000 kwa upande wa wanawake.

Hatua hiyo kwa Vivian inafungua ukarasa mpya katika ushiriki wake kwenye michuano ya dunia, kwani aliwahi kujaribu mara kadhaa na kuambulia medali ya fedha katika michuano ya mwaka 2003, 2005, 2007.

Mwanariadha kutoka nchini Ethiopia, Gelete Burka alitwaa medali ya fedha baada ya kushindwa kumpita Cheruiyot.

Medali ya shaba ilikwendea kwa mshiriki kutoka nchini Marekani Emily Infield ambaye alishinda baada ya kumpita mmarekani mwenzake Molly Huddle katika dakika za lala salama.

Upande wa wanaume katika mbio za kuruka maji na viunzi mita 3000, Conseslus Kipruto kutoka nchini kenya alichukua medali ya fedha, Brimin Kipruto akachukua medali ya shaba huku Jairus Kipchoge Birech alimaliza katika nafasi ya nne

Mpinzani wao raia wa marekani Evan Jagger aliona kivumbi wakati Wakenya hao walipotimka mbio.

Shelly-Ann Fraser-Pryce Kinara Wa Mita 100
Arsenal Vs Liverpool Hakuna Mbabe