Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamekutana na Wakuu wa Mikoa yote nchini,Jijini Dodoma na kuwapa semina ya kujenga uelewa wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi ili kurahisisha utekelezaji na usimamizi wa Mfumo huo katika ngazi ya mikoa na halmashauri zote nchini.

Akizungumza wakati wa semina hiyo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa wakuu hao wa mikoa ndio wasimamizi  wa shughuli zote na vipaumbele vya Serikali katika Mikoa yao hivyo wana jukumu kubwa la kuwahamasisha wananchi na wadau katika utekelezaji na matumizi ya mfumo huo na kuhakikisha ifikapo mwezi Aprili, 2022 asilimia 75 ya watanzania wawe na Anwani za Makazi na Postikodi katika maeneo yao ya makazi, maeneo ya biashara na ofisi

Kwa upande wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amesema kuwa mbali na vipaumbele vingi walivyonavyo katika Wizara hiyo Mfumo wa Anwani na Makazi ni muhimu haswa katika kuimarisha huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi

Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi Idara ya Uendelezaji Miji itahakikisha miji inapimwa na kupangwa vyema ili kurahisisha ufikishaji wa huduma mbalimbali za Serikali kwa jamii.

Rayvanny aweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza MTV EMA
Florent Ibenge afunguka maisha ya Clatous Chama