Msanii Rayvanny kutoka WCB Wasafi na mmiliki wa Next Level Music, Usiku wa kuamkia Nov 15, 2021, amefanikiwa kuweka rekodi ya kipekee ya kuwa msanii wa kwanza kutoka barani Afrika kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye hafla za utolewaji wa tuzo za MTV EMA 2021, Laszlo Papp Arena huko Budapest, Hungary.

Rayvanny ameshika nafasi kwenye vichwa vya habari mbali mbali Afrika kufuatia fursa hiyo aliyoipata kupitia mmoja wa wasanii mahiri wa muziki kutoka Columbia Juan Luis maarufu Malima aliyepata nafasi hiyo na kuamua kumpa fursa hiyo adhimu msanii Rayvanny.

Malima alikutana na Rayvanny na kuwa karibu zaidi baada ya kuachiwa kwa wimbo wake Tetema no 1, aliyomshirikisha Diamond Platnumz, ambapo wimbo huo ulimvutia sana msanii huyo kutoka Columbia aliyeamua kuingia makubaliano ya kuurudia wimbo huo kwa namna nyingine huku awamu hii yeye ndio akimshirikisha Rayvanny.

Wimbo huo ‘Mama tetema’ malima aliuachia rasmi Nov 12, 2021,  mpaka sasa umefikisha jumla ya watazamaji 3 Milioni kwenye mtadao wa youtube

Jr Junior atabiri mazito bifu la Diamond na Harmonize
Wakuu wa Mikoa wapigwa misasa anuani za makazi