Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana na Waziri Mkuu wa zamani wameungana na makada wengine wa chama hicho kumuombea kura mgombea Urais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kampeni Jimbo la Arusha mjini.

Kinana amemnadi Magufuli kwa kutimiza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 na kuwataka wananchi wa mkoa wa Arusha kumchagua tena ili aweze kutimiza ahadi mpya zilizotolewa na chama hicho.

”Nataka niungane na watanzania wenzangu kumuombea kuraMagufuli amefanya kazi kubwa nne, ya kwanza ametekeleza ilani kama alivyoahidi ametekeleza ahafdi zake wakati wakti anafanya kampeni, ametekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa ziara zake za mikoani, na amekuja na ahadi mpya zenye kurasa zaidi ya 300 kwa ajili ya kuwahudumia watanzania,” amesema Kinana.

Naye Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema kwa sasa mataifa mengine yana fujo kwa sababu ya mambo ambayo yanavuruga amani na kuwataka wananchi wampe zawadi ya kura kwa mazuri aliyofanya.

Maandamano yasababisha Mitihani kusimama Nigeria
Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Afrika nchini