Masheikh tisa wamesomewa Mashtaka katika Mahakama ya Kuu ya Kanda Arusha, imewahukumu kunyongwa hadi kufa Masheikh sita kati ya tisa waliokuwa wakishikiliwa kwa zaidi ya Miaka 10 katika Gereza Kuu la Kisongo.
Masheikh hao wamehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kulipua Kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph la Olasiti lolilopo jijini Arusha, Mwaka 2013.
Waliohukumiwa ni Imam Jaafar Hashima Lema, Yusuf Ali Huta, Hamadi Waziri, Abdul Hassa Masta, Kassim Idrisana Abashari na Hassan Omari huku waliochiwa huru wakiwa ni Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi.
Hata hivyo, Amani Mussa Pakasi alikamatwa na kurejeshwa tena Gerezani akikabiliwa na makosa mengine na katika hukumu hiyo, Jaji alionesha kuridhishwa na ushahidi wa Polisi kwamba Masheikh hao walilipua Kanisa hilo na kusababisha madhara.