Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza amekutana na kamati aliyoiteua kwa ajili ya kuhakiki mali za chama hicho.
Dkt.Magufuli alitangaza kamati hiyo tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma ikiongozwa na Dkt. Bashir Ally ikiwa na lengo la kuhakiki na kuchunguza mali za chama hicho.
“Nataka mali za chama zikinufaishe chama nataka mkamhoji mtu yeyote awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake.”, amesema Dkt. Magufuli.
Hata hivyo, Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Bashiru Ally amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi wanaozitumia mali za chama hicho kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa,
-
Lissu afanya muujiza, asimama kwa mara ya kwanza
-
Maneno: Wapinzani safari yao inaishia 2019- 2020
-
Msigwa awapongeza Askofu Kakobe na Gwajima