Baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotajwa kuwa waliukataa uteuzi wa rais John Magufuli kuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya tano wameeleza sababu za kuchukua uamuzi huo.

Mmoja kati ya wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe aliamua kuelezea. Aidai kuwa yeye ni mmoja kati ya wabunge ambao walipata nafasi ya kuteuliwa na rais lakini alihofia majukumu mazito na kasi ya rais Magufuli hivyo akaamua kujiweka kando.

“Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora nibaki na ubunge wangu,” Mbunge huyo alimwambia mwandishi wa gazeti la Mtanzania.

“Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi,”aliongeza.

Hadi sasa wizara nne za serikali ya awamu ya tano hazijapata mawaziri. Wizara hizo ni wizara Fedha, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Miundombino, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Mgombea wa CCM apinga Matokeo ya Lema, aeleza ‘figisufigisu’ zilizofanywa
Mwana FA: Wasanii wa Tanzania Tunaukosea Adabu Muziki