Kilio cha kuchezwa mfululizo Ligi Kuu ya Tanzania kimemfikia Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia ambaye amejibu mapigo kuwa imefikia hatua baadhi ya watu wanamtishia kuwa watamshtaki Shirikisho la Kimataifa (FIFA) ili afungiwe.

Licha ya hayo, Rais Karia amesisitiza kuwa Ligi hiyo haitasimama hata katika kipindi cha michuano ya Kombe la Dunia kwani inapotokea viporo yeye ndiye huwa anatukanwa.

Hata hivyo, ameiomba Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kuangalia namna ya kuweka ratiba katika kipindi cha Kombe la Dunia ili baadhi ya mechi zenye mvuto zisiingiliane.

“Hatutasimamisha Ligi maana sasa hivi natumiwa meseji tuaimamishe ligi lakini wakija watu wakapigwa viporo natukanwa mimi,”

“Baadhi wananitishia kwamba watanishtaki FIFA nifungiwe, Ligi yetu haitasimama wakati wa Kombe la Dunia kwa sababu hatuna timu inayoshiriki huko,”

“Lakini bodi ichukue tahadhari kwenye ratiba mechi zenye mvuto zitazamwe namna ya kuwekwa zisiingiliane, mfano unakuta anacheza Brazil na Argentina saa 1 jioni muda huo pia anacheza Simba SC au Young Africans,” amesema.

Chanzo: Mwanaspoti

Wizi wa pipikipi wasababisha mauaji watu 24
EAC kuzungumza kuhusu amani mashariki mwa DRC