Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amewaasa wananchi kuheshimu maeneo yanayobaki baada ya kumegewa sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Ileje Range yaliyowekewa mipaka.
Waziri Masanja, amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ya Kutatua migogoro ya ardhi akiwa katika Kitongoji cha Nkanka kilichopo Kijiji cha Itumba Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.
Amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia Kitongoji cha Nkanka kumegewa sehemu ya ardhi ya hifadhi na kuwataka wananchi kuacha kuendelea kuvamia eneo la msitu huo kwa ajili ya matumizi yao binafsi.
“Sasa niwaombe, huruma ya Rais isije ikawafanya mkajisahau, ninyi sasa hivi mtakuwa sehemu ya hifadhi mtasimamia na kuhakikisha miti haichomwi, haikatwi hovyo na shughuli za kibinadamu haziingii kwenye eneo hili la hifadhi” amesisitiza Naibu Waziri.