Takriban watu wanane wameuawa baada ya tukio la mashambuliano ya risasi kati ya vikundi viwili vya waasi katika mji wa vilima wa Chittagong uliopo nchini Bangladesh.
Mapigano hayo, yalitokea karibu na mji wa Ronwagnchhari, ambao ulisitisha safari za watalii tangu mwezi Oktoba (2022), wakati vikosi vya usalama vilipoanzisha msako dhidi ya kundi jipya la waasi lililoibuka la Kuki-Chin National Front -KNF.
Operesheni hiyo, ilipelekea mamia ya watu kulazimika kuyahama makazi yao na wengi wao wamejaribu kutafuta hifadhi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi yq India.
Mzozo katika vilima vya Chittagong uliodumu kwa miongo miwili na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, ulimalizika rasmi kwa makubaliano ya amani ya mwaka 1997, lakini bado vikundi vyenye silaha vinaripotiwa kuwepo katika eneo hilo.