Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amesema kuwa mapinduzi yoyote ya viwanda huanza na viwanda vidogo hivyo watu wasibeze dhana ya viwanda nchini.
Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akichangia mada kwenye kongamano la pili la kitaaluma la kuwasilisha matokeo ya tafiti juu ya mchango wa viwanda katika ukuaji wa uchumi endelevu.
“Maendeleo ya viwanda Tanzania kama ilivyo nchi nyingine yanatokana na kuwekeza nguvu katika viwanda vidogo, vya kati na hatimaye viwanda vikubwa na hakuna mapinduzi yoyote katika nchi kubwa yaliyoanza na viwanda vikubwa,”amesema Mhagama
Aidha, Mhagama ameongeza kuwa wapo watu wanaobeza viwanda vidogo na dhana nzima ya viwanda nchini ambapo amesema huo ni mtazamo finyu na umepitwa na wakati.
-
Tume ya uchaguzi yapokea taarifa kutoka kwa Spika Ndugai
-
Prof. Kitila Mkumbo ajiunga rasmi CCM
-
Balozi afunguka alivyomsafirisha ‘kijasusi’ Dkt. Shika
Hata hivyo, Mhagama amewaomba wananchi kuunga mkono sera ya viwanda kwa kuanza na viwanda vidogo kisha viwanda vya kati na hatimaye lengo la kuwa na viwanda vikubwa litatimia kupitia kuanza na viwanda vidogo