Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi wa Polisi, George Katabazi amewataka wale wote wanaomiliki Silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi au ofisi za serikali ya mtaa na kudai kuwa mwisho wa zoezi hilo ni Oktoba 20,2023.

Katabazi ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake, na kudai kuwa mara baada ya mwisho wa tarehe tajwa Jeshi la Polisi litafanya msako mkali, ili kuwabaini walio kaidi kusalimisha silaha hizo kwa hiari na hatua za kisheria zitafuata.

Mapema Septemba 20, 2023 pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, lilimesema kwa kipindi cha miezi sita limekamata makosa ya usalama barabarani 20,905 na kesi 47 zilifikishwa Mahakamani, ambazo ziliwakuta na hatia na kuwafungia Madereva wawili wa mabasi, kwa kosa la uendeshaji wa hatari.

Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi Mwaandamizi wa Polisi, David Misime Septemba 20, 2023 amefunga mafunzo ya siku mbili yaliyokuwa yakifanyika Mkoa wa Dodoma, yenye lengo la kuwabadilisha askari kutenda kazi zao kwa weledi na uadilifu pamoja na kuhakikisha wanafuata sheria za nchi na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Ukusanyaji Kodi: Maofisa KRA kupita nyumba kwa nyumba
Andre Onana: Ninakiri kufanya makosa