Taarifa za vyombo vya usalama nchini Kenya zimesema, Mhubiri tata Paul Mackenzie, aliajiri majambazi wenye silaha ili kusimamia zoezi la watu kujinyima chakula hadi kufa katika eneo la Shakahola.

Waziri wa usalama wa kitaifa wa nchi hiyo, Kithure Kindiki amesema hatua hiyo ilisimamiwa ipasavyo na kwama endapo mtu yeyote angebadili nia ya kutoendelea na mfungo huo angepigwa kwa kifaa butu au kunyongwa na majambazi hao chini ya usimamizi wa Makenzi.

Amesema mauaji katika msitu huo wa shakahola yametekelezwa katika kipindi cha siku 26 na kwamba atawafuta kazi na serikali kuwafungulia mashtaka maafisa wa usalama wote ambao walifumbia macho janga hilo.

Aidha Kindiki ameikosoa idara ya Mahakama kwa kumwachilia huru mara kadhaa mhubiri Paul mackenzie kwani anakabiliwa na makosa zaidi ya kumi na tano ya jinai ambayo yamefanyika katika shamba lake huku akisema baadhi ya miili ilikuwa imenyofolewa viungo.

Wawekezaji shirikisheni jamii Elimu, Afya - Alhaji Dkt. Mwinyi
Dkt. Kikwete, Marais wastaafu wakutana jukwaa la uongozi Afrika