Wakati mapigano mjini Khartoum yakiingia siku ya 23, raia waliobaki mjini humo wameelezea hali mbaya ya kikatili huku wakidai wanakaribia kuishiwa na mahitaji muhimu, masoko yakiwa yamefungwa na bidhaa kutoka nje haziingi tena.

Moja wa wafanyabiashara hao, Yousif Ahmed amesema hali ni mbaya na kwamba watu wanalazimika kuiba ili kuokoa uhai wao kutokana na kukosa mahitaji muhimu.

Amesema, “tunalazimika kuiba ili tupate riziki ya kujikimu kwa siku na siku zijazo, sasa kila kitu kimepotea, tunateseka sana kutokana na janga hili, watu wote inawalazimu kuiba kila wiki.”

Ahmed amesema, ukosefu wa usalama mjini humo pia unamaanisha kuwa wafanyabiashara wanapaswa kubuni njia mbadala za kulinda bidhaa zao, ili kuepuka kuibiwa.

Umoja wa Mataifa unasema, takriban Wasudan milioni 19 wanaweza kuathiriwa na uhaba wa chakula kutokana na mzozo huo.

Wanadiplomasia wakosoa kukosekana kwa utashi Afrika
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 26, 2023