Wanadiplomasia wa Kiafrika, wamekosoa kukosekana kwa utashi miongoni mwa viongozi wa Afrika, kusuluhisha mizozo barani humo. Wameyaeleza hayo sambamba na maadhimisho ya miaka 60 tangu kuundwa kwa umoja wa Afrika huru.

Jumuiya ya wanadiplomasia kutoka Afrika walioko nchini Uganda imeadhimisha Siku ya Afrika kwa kutoa mwito wa kukomeshwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan. Wanaelezea hali hiyo kuwa ya kusikitisha na wamewataka viongozi wa Afrika kuonesha nia ya dhati na kuchukua hatua madhubuti kurejesha amani katika nchi hiyo na kwingineko.

Tarehe 25 Mei ni siku ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika uliokuja kuwa Umoja wa Afrika ambao lengo lake lilikuwa ni ukombozi wa bara hilo.

Wanadiplomasia na wazalendo wa Afrika waliojitokeza kuadhimisha siku hiyo mjini Kampala wamewataka viongozi wa Afrika wasisubiri wageni kuja kutatua mizozo kama kama ule wa Sudan.

Tanzania, Afrika Kusini kuadhimisha siku ya Afrika
Tunalazimika kuiba ili kupata mahitaji - Wakazi wa Sudan