Baraza la Wanawake wa Chama CHADEMA – BAWACHA, limemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuandika historia kwa kuwezesha zoezi la upatikanaji wa Katiba mpya na kumataka kutokutaka tamaa kwani wanaopinga jambo hilo wanamjaribu.

Ombi hilo, limetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA – BAWACHA, Catherine Ruge hii leo Machi 8, 2023 katika Kongamano lililoandaliwa na BAWACHA na kufanyika ukumbi wa Kuringe uliopo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi ni Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chama CHADEMA – BAWACHA, Catherine Ruge.

“Tunafahamu unafanya jitihada kubwa na Mwenyekiti Mbowe kuhakikisha tunapata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, usiogope hujuma za wanaotaka ushindwe kama wao walivyoshindwa huko nyuma,” amesema Catherine.

Aidha, ameongeza kuwa, watu hao wanaopinga jitihada za Rais za kupatikana kwa katiba mpya wana nia ya kumpima Kiongozi huyo wa nchi, na hivyo kumtaka aendeleze jitihada za kulijenga Taifa salama na lenye mshikamano.

Mimi ni Rais wa Watanzania wote: Rais Samia
Ajali nyingine Geita: Basi lapinduka saba wafariki