Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna haja ya kuwakamata watu wanotumia mitandao ya kijamii vibaya, ambapo ameshutumu wale wanaosambaza habari kwenye mitandao kuwa yeye amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais Museveni amesema kwamba wale wanaohusika na habari kama hizo wanapaswa kusakwa na kukamatwa kwa kuwa wamekuwa wakipotezea watu muda wao.

”Nataka wawafuatilie kwa haraka wale wanaozua uvumi kama huo”amesema Museveni.

Katika mtandao wa Twitter Kumekuwa na uvumi katika siku za hivi karibuni kwamba kiongozi huyo alikuwa amesafirishwa kutoka nchini Uganda na kupelekwa nchini Ujerumani akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua maradhi ya tatizo la kupumua linalohusishwa na ugonjwa wa corona.

Rais Museveni amesema kwamba wale wanaozua habari kama hizo wanapaswa kufuatiliwa na vyombo vya usalama ili kukamatwa haraka iwezekanavyo.

Kesi uchaguzi wa TFF kuunguruma leo
Kesi ya Guelor Kaku yawekwa kapuni CAF