Tunaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 07 mjini Tanga na kinyang’anyiro kikitarajiwa kuwa kwenye nafasi ya ujumbe tu baada ya ile ya urais kubaki na mgombea mmoja pekee, Wallace Karia anayetetea kiti chake cha Uraria.

Sasa wakati mchakato wa uchaguzi ukiendelea leo Ijumaa (Julai 09) Jaji Edwin Kakolaki atasikiliza kwa mara ya pili kesi ndogo iliyofunguliwa na Ally Salehe ambaye alienguliwa kwenye mchujo wa awali kuwania urais kwenye uchaguzi huo kwa kutokidhi takwa la kikanuni.

Baada ya kuenguliwa Salehe alifuungua kesi Mahakama Kuu kupinga katiba ya TFF na kesi ndogo ya kuomba zuio la mchakato wa uchaguzi huo.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilisikilizwa Julai 3 kabla ya Jaji Kakolaki kuiahirisha hadi Julai 9 (leo) ambapi itasikilizwa kwa mara ya pili kabla ya kutolewa hukumu.

Mwanasheria Frank Chacha anayemtetea Salehe alisema kesi ndogo itasikilizwa leo na ile ya msingi ya kupinga Katiba ya TFF itasikilizwa Julai 16.

Simba SC yasajili beki 'KIMYA KIMYA'
Wanaozusha taarifa hizi wakamatwe - Rais Museveni