MKATABA WA YANGA vs AZAM USITUMIKE KUBEZA BILIONI 20 ZA MO DEWJI vs SIMBA

Baada ya Klabu ya Yanga na Azam kuingia kandarasi ya kurusha maudhui yao kwa thamani ya 34B, naona watu wengi wameanza kubeza Uwekezaji wa Tajiri Mo Dewji wa kiasi cha 20B ndani ya Simba SC Tanzania kuwa ni wa milele.

Sasa ngoja tuwajibu kwa hoja;

Kwanza Mo Dewji hajasaini mkataba na Simba, ndio kwanza mchakato uko mbioni kukamilika, hivyo hiyo milele unayoisema labda ni mnajiombea moto wa milele wenyewe. Na hata ukikamilika Ni lazima kutakuwa na ukomo wa muda.

ANACHOKIFANYA MO DEWJI NI KUKUZA CHAPA YA MNYAMA. HIi maanake ni sawa na anaiongezea thamani klabu kabla hajawekeza ili kum assure return ya pesa yake pindi atakapomwaga minoti yake, Tukumbuke Mpira ni biashara.

Kiaje?, twende sawa!.

  1. Hilo dili walilosaini Yanga, Simba nao watalisaini siku sio nyingi, kinachosubiriwa ni makubaliano ya pande mbili juu ya kiasi kinachohitajuka. Na hata kama litakwama basi kuna kampuni nyingine itapewa kandarasi hiyo kwa pesa wanayotaka Simba.
  2. Kiasi walichosaini Yanga kilikataliwa na Simba kwa sababu hakiendani na thamani ya klabu kwa sasa. Yaani timu iliyoingia top 10 za klabu za Afrika kwa msimu wa 2020/2021 ilipwe sawa na timu ambayo hata top 50 haipo?. Hivyo Azam wanajipanga kutoa donge nono zaidi ya walilomwaga pale Jangwani. MNABEZAJE?
  3. Mo Dewji kabla hajaweka 20B pale Msimbazi tayari anatoa pesa ya ziada kufadhili timu katika masuala ya usajili, mishahara, kambi n.k. Ufadhili huu umesaidia timu kufanya vyema ndani na nje ya uwanja. Yaani MNABEZA?
  4. Uongozj wa Mo Dewji umesaidia Simba kusaini kandarasi ya 2B ili kutengeneza jezi toka 100M ya awali. Pale Jangwani Mapato ya mauzo ya Jezi kwa mwaka 2019 na 2020 timu ilivuna chini ya 60M. Bado MNABEZA?
  5. Azam media wamemwaga 34B pale Yanga kwa duration ya miaka 10 lakini Mo Dewji anatarajia kutoa 20B kwa mkupuo. Hebu tuwe serious guys. Hivi mnaanzaje KUBEZA?
  6. Ufadhili huu wa Mo Dewji kabla ya kuweka 20B, umeiwezesha Simba kuvuna 2.5B kwa kufika hatua ya robo fainali katika msimu wa 2020/2021, kumbuka hii ni mara ya 2 ndani ya misimu 3 ndani ya Afrika Mashariki. Hivi mko serious KUBEZA?
  7. Ndani ya miaka mitatu Simba imekuwa klabu inayofuatiliwa na watu wengi zaidi katika mtandao ya kijamii kuliko timu zote Afrika Mashariki na baadhi ya timu kubwa za Afrika. Sitoshangaa kuona donge la kurusha maudhui yake likianzia 50B+. Ndiyo Tutaacha KUBEZA.

NB:
Simba, chini ya Mo Dewji imechangia kwa 90% kwa Tanzania mpaka kupata sifa ya kuwakilishwa na timu nne katika mashindano ya kimataifa msimu ujao wa 2021/2022.

Credit kwa Sportkitaa

Kesi ya Guelor Kaku yawekwa kapuni CAF
Kaseja: Kwa hapa Tanzania hakuna kama Simba SC