Kamati ya Rufaa ya CAF imetupilia mbali Rufaa ya DR Congo kuhusu mkanganyiko wa uraia wa kiungo Guelor Kanga Kaku raia wa Gabon.

DR Congo walikata Rufaa kwenye kamati hiyo baada ya kamati ya nidhamu ya CAF kumuidhinisha Kanga kuwa raia wa Gabon na si DR Congo ambao walilamika kuwa nyota huyo amedanganya umri kwa kusema alizaliwa 1990 nchini Gabon.

Madai ya DR Congo yalieleza kuwa mama wa mchezaji huyo alifariki mwaka 1986 nchini kwao.

Katika malalamiko hayo DR Congo walishindwa kuwasilisha ushahidi halisi kwenye kamati ya rufaa ya CAF.

Hatua hiyo imeifanya Kamati ya rufaa ya CAF kutangaza maamuzi ya kuyaweka kapuni malalamiko (Kesi) ya DR Congo dhidi ya Kanga Kaku.

Wanaozusha taarifa hizi wakamatwe - Rais Museveni
Bilioni 20 za Mo zazua tena mjadala mitandaoni