Boniface Gideon, Muheza – Tanga.

Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema – BAWACHA, Wilaya ya Muheza limefanya mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wa kutambua fursa za Kiuchumi na matumizi sahihi ya fedha kwa Wanawake Wajasiriamali Wilayani humo, wakilenga kuwafikia Wanawake zaidi ya 5,000.

Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Kanda ya Kaskazini, Yosepha Komba aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo Kiuchumi Wanawake nakuwafanya kuwa imara Kiuchumi na kupunguza utegemezi katika Jamii,

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini, Yosepha Komba Akizungumza na Wanawake Wajasiriamali Wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Kiuchumi yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake chama hicho – BAWACHA, Wilayani humo.

Amesema, “Kama tunavyofahamu Chama chetu kinawategemea Sana Akinamama na Chama Kinawathamini Akinamama hivyo kwakuona hilo tumeona kuwapatie Mafunzo maalumu ya Ujasiriamali ili wainuke Kiuchumi lakini pia wakienda huko wakatoe Elimu hii kwa wengine.”

Sehemu ya Washiriki katika mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo, George Chambai alisema changamoto kubwa zinazowakumba Wanawake Wajasiriamali nikuchukua mikopo Umiza ambayo inawafanya kurudi nyuma Kiuchumi,na kuwataka Wanawake kuwekeza fedha kidogo kidogo, ili wapate fedha za akiba ,

“Sisi wataalamu wa uchumi tunawashauri watumie njia m’badala kupata mitaji ikiwemo kuwekeza kidogo kidogo na kama wanataka mikopo waende kwenye Taasisi za kifedha kama Benki na wapatiwe Elimu kabla ya kuchukua mkopo” Alisisitiza Chambai.

Hakuna mwenye msuli wa kuligawa Taifa - Dkt. Samia
Tanzania, Comoro kushirikiana Sekta za Afya, Uchukuzi