Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Kagimbo Bakari amesema Jeshi hili limewakamata wahamiaji haramu wanne raia wa Cameroon, ambao wamedai wapo nchini  kwa ajili ya kufanya majaribio ya  kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports zilizopo jijini Tanga.

Amesema hayo wakati aitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo amesema wahamiaji haramu hao wamedai wameletwa na wakala aitwaye Benard Matomondo Mfaume.

Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Kagimbo Bakari

Aidha amesema kuwa waliingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90, badala ya visa za kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.

Hata hivyo alibainisha kuwa mara baada  ya kuwakamata raia hao, waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal, ambao walikana kuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua walizokuwa nazo zote ni za kughushi na pasipoti walizokuwa nazo sio sahihi.

Waziri kufichua wanao nufaika na ujambazi
Wauguzi mbaroni kwa kuuza dawa