Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35-40 amenusurika kifo baada ya kujitumbukiza kwenye kisima cha Maji kilichopo mtaa wa Mazense A’ Wilayani kilosa Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamesema mtu huyo alifika katika kisima cha kwanza na kukuta watu wakichota Maji kisha kutaka kuzama lakini wananchi walimkataza na baadaye aliondoka kwenda kisima cha pili na kutumbukia.

Kisima cha maji.

Wamesema, “alikuja hapa akakuta kuna mdada anafua alichukua kopo lake yake kisha alitaka kujitupa kisimani tukamkataza badae tukasikia watu wanasema kuna mtu ametumbukia kisimani tukamkuta baba yuleyule tuliyemkataza mwanzo ametumbukia.”

Mwenyekiti wa mtaa wa Mazensa A, Mashaka Ally amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema walifanikiwa kumuokoa mtu huyo akiwa hai, kisha kumuwahisha Hospitali na kisa cha kujirusha mtoni bado hakijafahamika.

Balozi Kombo awasilisha hati za utambulisho nchini Malta
Dhahabu ya kinyemela yachukua uhai wa Wachimbaji saba