Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha vifo vya Wachimbaji wadogo saba ambao wamefariki baada ya shimo waliloingia kwa ajili ya kazi yao kujaa maji.

Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia hii leo Machi 11, 2023 katika Kijiji cha Igando, kilichopo Kata ya Magenge Wilaya na Mkoa wa Geita.

Amesema, wachimbaji hao waliingia katika eneo lililofungwa kwa sababu za kiusalama na uwepo wa mvua za masika lakini waliingia kinyemela majira ya usiku, na tayari miili ya wachimbaji wote imeopolewa na kutambuliwa.

Aidha ameongeza kuwa, “migodi ambayo haikuwa vizuri kiusalama na hizi mvua zinazonyesha mashimo yalijaa maji, walikuwa wanaingia usiku wakazidiwa na maji wakashindwa kutoka na kupelekea umauti wao.”

Taharuki: Anusurika kifo kwa kujirusha kisimani
Rais Samia aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Dodoma