Kiungo kutoka nchini Kenya, Victor Mugubi Wanyama, atakaa nje kwa kipindi cha majuma sita baada ya kufungiwa michezo mitano.

Southampton itakuwa bila ya kiungo wake mashuhuri Victor Wanyama kwa kipindi hicho, baada ya chama cha soka nchini England FA, kuthibitisha kwamba kadi nyekundu aliyoonyeshwa kiungo huyo wakati wa mchezo dhidi ya West Ham inamfanya kufungiwa michezo mitano.

Hii ni mara ya tatu kwa Mkenya huyo mwenye miaka 24 kutolewa nje msimu huu, hivyo michezo mitatu aliyofungiwa na miwili ambayo inatokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa inakamilisha michezo mitano.

Wanyama alipewa kadi hiyo baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo mshambuliaji wa West Ham Mfaransa Dimitri Payet.

Wanyama alitolewa nje baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Bournemouth mwezi November mwaka jana, vivyo hivyo kwenye mchezo dhidi ya Norwich mwanzoni kabisa mwa mwezi January.

Punde tu akimaliza adhabu yake, kikosi cha Southampton kitakabiliana na Liverpool mwezi Machi 19.

 

 

Mabingwa Wa Tanzania Bara Kuwafuata Sekho De Joackim
Azam FC: Si Rahisi Kubadilisha Mfumo Kwa Sasa