Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni leo wametoka nje ya Bunge wakisusia vikao vinavyoendelea wakipinga maamuzi na uendeshaji wa vikao vya Bunge hilo unaofanywa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Bunge, katika kikao walichofanya na wabunge hao, Kiongozi wa Kambi ya UPinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema kuwa Naibu Spika ni tatizo la Msingi la Bunge la Kumi na Moja.

“Na nanipendekezo langu kwa wabunge wa Kambi ya Upinzani kwamba tatizo kubwa la Bunge la Kumi na Moja, la Msingi kabisa ni Naibu Spika. Kwamba kwa sababu tumeona mara kwa mara Bunge linavurugika, mienendo ya Bunge inavurugika, maamuzi ya Bunge yanapuuzwa… ni tangu ujio wa mtu huyo mpya Dk. Tulia Ackson,” alisema Mbowe.

“Mimi ni pendekezo langu kwa Wabunge leo, la kwanza kabisa tujadili ajenda ya kutakuwa na imani na Naibu Spika. Na katika kutokuwa na imani na Naibu Spika, nitapendekeza kwenu waheshimiwa Wabunge, kwamba siku yoyote ambayo Naibu Spika huyu atakuwa kwenye kiti, sisi tutatoka nje,” aliongeza.

Mgogoro huo ulianza jana baada ya Naibu Spika kukataa kuruhusu Bunge kukatisha mjadala uliokuwa unaendelea ili kujadili suala ya kufukuzwa kwa wanafunzi zaidi ya 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hali iliyopelekea mtafaruku na kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.

Vicente del Bosque Ataja Kikosi Chake Cha Mwisho
Audio: Raymond aeleza alivyoshiriki kuandika 'hits' za Diamond, Janjaro