Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Ntime Mwalyambi amefungua Mafunzo ya wawezeshaji mfumo wa Mshitiri kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

Ufunguzi huo, umefanyika hii leo Machi 22, 2023 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambapo Mwalyambi amesema washiriki watapata uelewa wa kutosha na kuwezesha utekelezaji utakaoimarisha utaratibu sahihi wa manunuzi ya bidhaa za Afya kwa kuzingatia Mfumo wa Mshitiri.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa Mshitiri.

Amesema, “washiriki wanatakiwa kujifunza kwa bidii na weledi mkubwa ili kupata uelewa wa kutosha na kuwezesha utekelezaji utakaoimarisha utaratibu sahihi wa manunuzi ya bidhaa za Afya kwa kuzingatia Mfumo wa Mshitiri.”

Kikao hicho, kimewahusisha Mganga Mkuu wa Mkoa, wawakilishi wa Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, wakufunzi wa kutoka TAMISEMI, Watendaji ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na Wanahabari.

Wawekezaji 23 waonesha nia Kongani ya kisasa Viwanda
Treni SGR kuharakisha ukuzaji shughuli za kimaendeleo