Licha ya uzalishaji mkubwa wa zao la chai unaofanywa na Wakulima nchini, Watanzania wengi wamekuwa wakichwa chai daraja la nne hadi la tano kutokana na jinsi bidhaa inavyochanganywa na watu kuangalia gharama badala ya ubora.

Hayo, yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Dar24 Media Stanslaus Lambat ofisini kwake jijini Dodoma hivi karibuni na kuongeza kuwa hatua hiyo inatokana na mapungufu na muda uliopo katika viwanda vya ndani.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Amesema, “chai ambayo tunaiona hapa mtaani ni chai ambayo ni ya grade ya chini, kwa maana ya kwamba wanachanganya zile gredi za chini kutupatia chai, na uhalisia wa soko letu nchini asili yake huwa ni bei sio ubora na kama nchi sasa tumeanza kuchukua hatua.”

Waziri Bashe amesema, kwa mwaka jana (2022), ilitarajiwa soko liwe limeanza la kuuzia chai nyumbani lakini ilishindikana na kwamba ana imani kwa mwaka huu soko hilo linaweza kuanza ili kuhakikisha chai inakuwa na ubora kulingana na mahitaji na soko la uhakika.

Simba SC yarejea Dar, wachezaji wapewa mapumziko
Saba mbaroni tuhuma za mauaji ya Hakimu