Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema atamlinda mtumishi wa umma kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa atakayefanya kazi kwa bidii na uadilifu kumuondoa yeyote yule ambaye atazembea kazini.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga, katika ziara yake ya kikazi huku akiwahimiza kufanya kazi kwa weledi na kuisaidia Serikali kupiga hatua za kimaendeleo.

Amesema, “kuna watu wanafanya kazi kwa moyo wao wote na wanatimiza majukumu yao ipasavyo kwa weledi wa hali ya juu hawa nitawalinda na kuwakumbatia na kuhakikisha wanapata stahiki zao zote wanazostahili kwa wakati lakini wale wazembe na wabadhilifu nitawatoa kwenye nafasi zao.”

Hata hivyo, Mchengerwa ameongeza kuwa, “mshikamano baina ya chama na serikali ni muhimu sana hivyo lazima tufanye kazi za serikali vizuri, ili chama kiendelee kuwa madarakani.”

Muunganiko wapinzani, waasi waitikisa Serikali DRC
Ajali ya Ndege: Mkuu wa Mkoa atoa ufafanuzi