Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka ametoa wito kwa watumishi wa umma kubadili mtindo wa maisha kwa kujihusisha na michezo mbalimbali, ili kulinda afya zao na hivyo kutoa mchango wao kikamilifu katika kuwahudumia wananchi.

Dkt. Moses Kusiluka, ametoa wito huo jijini Dodoma katika bonanza la Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kupitia hotuba iliyowasilishwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Ikulu, Majura Mahendeka.

Bonanza hilo ambalo limehusisha matembezi mepesi kwa viongozi na watumishi wa serikali kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za serikali kutoka viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, ikiwa ni sehemu ya maandalizi yamashindano ya SHIMIWI, yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mkoani Iringa.

Akimwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Mahendeka ameanisha baadhi ya majukumu ya msingi ya watumishiwa serikali yakiwemo kutoa huduma bora kwa wananchi, kufanya kazi kwa bidiii na weledi, kuongeza tija na ubunifupamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali za utumishi wa umma.

“Watumishi wa umma tutambue kwamba sisi ndio chachuya maendeleo ya Taifa kwani ndio tunahusika na kupanga mipango yote ya maendeleo ya nchi pamoja na utekelezajiwake. Ili kutekeleza haya yote, watumishi wa umma hatuna budi kuwa na afya njema na akili timamu kufanya mazoezi na kuepuka matumizi ya vyakula na vinywaji vinavyoweza kuathiri afya,” amesema Katibu Mkuu Mahendeka.

Akiwasilisha salamu toka Wakala wa Usalama na AfyaMahali pa Kazi – OSHA, Taasisi iliyodhamini bonanza hilo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Khadija Mwenda amesema udhamini huo ni sehemu kuhamasisha uwepo wa programu za michezo kwenye maeneo ya kazi zinazolenga kushughulikia changamoto hatarishi za kisaikolojia zinachoyakumba maeneo mengi ya kazi.

“Ulimwengu wa kazi unakabiliwa na vihatarishi mbali mbaliikiwemo kihatarishi cha kisaikolojia (psycho-social hazard) ambacho kinapelekea matatizo mengi kwa wafanyakazikama vile ajali na magonjwa mbali mbali yakiwemo yaleyanayoathiri afya ya akili, kumekuwa na ongezekola magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama vile: Shinikizo la Juu la Damu, Kisukari na Saratani,” amesema.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA, kwa takwimu zilizokusanywa katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini katika mwakawa fedha 2022/2023, jumla ya wafanyakazi 316,000 walipimwa afya na madaktari wa OSHA ambapo kati yao, wafanyakazi 126,400 sawa na 40% walikuwa na uzitouliozidi wastani na wafanyakazi 15,800 sawa na 5% walikuwa na Shinikizo la Juu la Damu.

“Takwimu hizi ni kiashiria kuwa wafanyakazi wengi wapokatika hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza ambayo madhara yake hayaishii tu kwa mfanyakazimwathirika bali hupelekea hasara kwa familia na Taifa zima kwa ujumla kwa kupoteza nguvukazi,” amesema Mwenda.

Kutokana na ukubwa wa changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza na athari zake katika uchumi wa nchi, Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA ametoa rai kwa waajiri nawafanyakazi kuendelea kuzingatia ushauri ambaoumekuwa ukitolewa na wataalam wa OSHA baada yakufanya ukaguzi na kuchunguza afya za wafanyakazikwenye maeneo ya kazi ikiwemo kuanzisha programu za michezo mahali pa kazi.

lbrahim Sangare avigonganisha vigogo Ulaya
Cadena afichua siri nzito kwa Ally Salim