Wazee wa Chama cha ACT- Wazalendo Mkoani Kigoma wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya Chama hicho, Alhaj Jaffar Kasisiko wamesikitishwa na kauli aliyotoa Spika Ndugai kuwa anaweza kumzuia Zitto Kabwe asiongee chochote mpaka ubunge wake utakapokwisha
Katika taarifa iliyotolewa na Wazee hao imesema kuwa kitendo cha Spika kumzuia Zitto Kabwe kuongea bungeni ni sawa na kuwazuia wao wasiongee na shida zao zisiweze kutatuliwa.
“Inaonekana kauli hiyo imeshafanyiwa kazi na kitendo cha kumwita Zitto kwenye Kamati ni sawa na kupoteza muda, jambo hilo halimtendei haki kijana wetu Zitto Kabwe na sisi wenyewe,”amesema Mzee Kasisiko.
Aidha wazee hao wamemtaka Spika Job Ndugai na viongozi wengine watazame mambo ambayo yanawaunganisha wananchi na viongozi kwa pamoja ili waweze kujiletea maendeleo katika jamii.
-
Mdee alivimbia jeshi la polisi, agoma kuripoti kwa DCI
-
Mbunge wa CCM aliyemkodia ndege Lissu atoboa siri
-
Kubenea augua ghafla Dodoma
-
CCM wampongeza aliyekodi ndege ya Lissu
Hata hivyo, Wazee hao wamesema kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi waliomchagua Mbunge huyo.