Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka watumiaji wa eneo lililotolewa kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kilimo waendelee kulilinda eneo lililobaki kwa ajili ya Hifadhi ya Bonde la Mto Usangu.

Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na wadau, wawekezaji wa Bonde la Usangu, wakulima wa mpunga, wamiliki wa mashine za kukoboa mpunga na wafugaji Januari 16, 2023 Mkoani Mbeya.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana.

Amesema, “Tusifuge wala kulima katika eneo lililobaki eneo hili ni chanzo kikubwa cha maji na sehemu ya utalii tuendelee kulitunza eneo hilo kwa ajili yetu na vizazi vijavyo hii ni rasilimali yetu sote tuilinde.”

Akiwa katika eneo hilo, naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo aaliwataka watumiaji wote wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji, kuheshimu sheria ya mazingira.

Kamati ya Bunge yapokea taarifa ya Ofisi Makamu wa Rais
Mtoto wa Rais akamatwa kwa amri ya kaka yake