Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuwasilisha taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 15,000 yanayotambulika na wananchi kama Madarasa ya Mama Samia ifikapo tarehe 25 Januari,2022.

Akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Tume ya walimu leo Jijini Dodoma Waziri Bashungwa amewataka wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanajiridhisha na taarifa hizo kiundani zaidi kwa kuangalia utaratibu uliotolewa na Serikali ulifuatwa

Waziri Bashungwa amewataka kutumia ujuzi walionao katika kupitia taarifa hizo kiundani zaidi kabla hazijawasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kujirizisha na miongozo iliyotolewa na Serikali na kuangalia dhamani ya fedha iliyotolewa imeenda sambamba na ubora wa madarasa yaliyojengwa.

Ameendelea kusema kuwa ujenzi wa madarasa 15,000 kumesaidia kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya kidato cha kwanza , hivyo ameiagiza Tume kuhakikisha walimu wanapewa fursa ya kufundisha watoto, wanakuwa wanamaadili mema ili kupata matokeo chanya kwa wanafunzi wanaowalea.

Wanawake wapigwa marufuku kukaa mbele kwenye malori
Waziri Mazrui:Ulawiti Zanzibar ni tatizo (Video)