Mshambuliaji wa kutumainiwa katika kikosi cha Young Africans kinachoshiriki michuano ya Kombe la Kagame Wazir Junior amesema amejipanga kuitumia michuano hiyo ili kurudisha makali yake.

Waziri Jr ametoa kauli hiyo baada ya kuifungia Young Africans bao la kuongoza dhidi ya Nyasa Big Bullets jana Jumapili (Agosti 01), Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Amesema dhamira yake kuu kwenye michuano hiyo inayoendelea jijini Dar es salaam, ni kumaliza kinara kwenye orodha ya ufungaji bora.

“Young Africans kwa asilimia kubwa ya wachezaji wamepumzika, hapa tumechanganyika kwa hiyo kuna ugumu utakaokuwepo ila tutapambana kuhakikisha timu inafanya vizuri,”

“Kwa upande wangu pia nitahakikisha ninatimiza malengo yangu ya kuwa mfungaji bora.” amesema Junior.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Young Africans wamekwenda mapumziko baada ya kumaliza msimu wa 2020/21 Tanzania Bara, huku benchi la ufundi likiwa na mabadiliko kwa kuongozwa na Kocha wa Makipa Razaq Siwa.

Kocha Mkuu Nasrideen Nabi na wasaidizi wake nao wamekwenda mapumziko nchini kwao Tunisia.

Majaliwa azindua mafunzo ya uanagezi awamu ya 3
Ambokile anarudi Mbeya City