Mshambuliaji Eliud Ambokile anatajwa kuwa mbioni kurejea Mbeya City FC, akitokea nchini Zambia.

Ambokile aliondoka Mbeya City misimu miwili iliopita na kutimkia DR Congo kisha alielekea Zambia kucheza soka la kulipwa.

Taarifa zinaeleza kuwa, Mshambuliaji huyo mzawa atasaini Mbeya City FC kama mchezaji huru.

Ambokile alijiunga TP Mazembe akitokea Mbeya City FC kisha kutimkia Nkana FC na kote mambo yalimuendea ndivyo sivyo.

Hatua hiyo inamfanya arudi nyumbani kuisaidia timu yake ya Mbeya City, baada ya mabosi wake wa zamani kumuomba afanye hivyo.

Hata hivyo Mshambuliaji huyo amejipanga kuitumia Mbeya City kujiweka sawa, na amekiri hajakata tamaa kucheza nje ila michongo haijakaa sawa.

Waziri Jr ataka kiatu Kagame CUP
Serikali yakabidhi ambulance boats 2 Mwanza