Waziri Mkuu wa Burkina Faso, Dkt. Albert Ouédraogo amewatembelea manusura wa shambulio la msafara wa usambazaji unaoongozwa na jeshi, wakiwemo raia, madereva na wafanyabiashara.

Katika shambulio hilo, watu 35 waliuawa na wengine 37 kujeruhiwa wakiwemo watoto 12 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Watoto ya Charles-de-Gaulle huko Ouagadougou.

Waziri Mkuu huyo pia alikutana na baadhi ya raia ambao walimsimulia tukio hilo kuwa liliuwa 35 baada ya kilipuzi cha kutengenezea kugonga msafara huo katika eneo la Djibo na Bourzanga kaskazini mwa nchi hiyo kilichorushwa na wanajihadi.

Awali, akitoa heshima kwa manusura na majeruhi, rais wa Burkina Faso, Paul-Henri Sandaogo Damiba aliapa kuwashinda waasi hao akisema wamekuwa na roho ya kinyama na huo ni uthibitisho kwamba lazima waendeleze mapambano dhidi ya wale wote wanaokataa kufuata njia iliyonyooka.

Kikosi tawala cha Burkina, ambacho kilichukua mamlaka mwezi Januari, kilitangaza vita dhidi ya waasi kuwa kipaumbele cha kwanza na mapema siku ya Jumapili jioni, ikiwa siku moja kabla ya shambulio hilo, Damiba alikaribisha “utulivu wa jamii” katika maeneo kadhaa.

Hata hivyo, Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa kuzidi kwa “vitendo vya kukera” vya jeshi la nchi hiyo kunalazimisha mchakato wa mazungumzo na baadhi ya makundi yenye silaha, kupitia viongozi wa kidini na wa mitaa.

Wakili amtaka Waziri kutimiza ahadi mapendekezo ya wadau wa Habari
Serikali 'yawabana koo' Wakandarasi ujenzi miradi ya Maji