Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji safi na tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200,000 ambao utahudumia vijiji viwili vya Mkongotema na Magingo katika kata ya Mkongotema, wilayani Songea, mkoani Ruvuma.

Aidha, Majaliwa amewapongeza wakazi hao kwa kukubali kuchangia ujenzi wa mradi huo kwani katika baadhi ya maeneo miradi kama hiyo imekwama kukamilika kwa sababu wananchi waligomea kuchangia.

“Mradi huu ni lazima tuutunze kwani hali ya hewa imebadilika sana hivi sasa, sababu ni sisi wenyewe wananchi ambao tumekata miti sana ili kupanua maeneo ya kilimo, Mtazamo wetu katika Serikali hivi sasa ni kulima kwenye eneo dogo lakini mavuno yawe mengi,” Amesema Majaliwa.

Aidha, amewaomba wakazi wa vijiji hivyo watunze akiba ya chakula walichonacho kwa sababu hali ya hewa imebadilika na hakuna anayejua mvua itaanza kunyesha lini.

 

Gambo awabebesha zigo Wakuu wa Wilaya Arusha
Shaka awataka watendaji UVCCM kujitathmini