Tume ya Utumishi wa Umma nchini Kenya imemuondolea Waziri wa Elimu Profesa George Magoha mamlaka ya kusimamia watumishi katika sekta hiyo.
Hii inakuja siku chache baada ya Profesa Magoha kuonekana akimfokea, kumdhalilisha na kumtukana hadharani Mkurugenzi wa elimu wa kaunti ya Gishu Gitonga Mbaka, jambo ambalo wengi hawakufurahia.
Profesa Magoha hakuomba msamaha kwa kumkosea heshima Mkurugenzi huyo mbele ya maafisa wadogo, akisema huo ndio mtindo wake wa kufanya kazi.
Tume hiyo imesema Katibu wa Wizara hiyo anayesimamia Elimu ya Msingi Dokta Bello Kipsang, atashugulikia masuala yote ya watumishi wa Elimu kuanzia sasa hadi itakapotangazwa.