Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman amejiuzulu ghafla akilalamika dhidi ya makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na wanamgambo wa Hamas.
Uamuzi wa kujiuzulu wa Avigdor Liebermann unaidhoofisha serikali ya mseto ya waziri mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu na huenda ikapelekea kuitishwa kwa uchaguzi kabla ya wakati.
Aidha, Liebermann amesema kuwa makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na viongozi wa Gaza ni sawa na kusalimu amri mbele ya ugaidi baada ya siku mbili za mapaigano makali.
Waziri huyo alitaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wanamgambo wa Hamas ambao wamekuwa wakifyatua makombora dhidi ya Israel hivyo uamuzi wa makubaliano ya kusitisha mapigano hajakubaliana nao.
Hata hivyo, serikali ya Bejamin Netanyahu inalaumiwa kuanzia ndani ya chama chake, pia katika miji inayoshambuliwa kwa makombora ya wanamgambo wa Hamas.