Watu saba wameuawa katika matukio mawili tofauti ya kupigwa risasi katika shamba la uyoga na katika kampuni ya lori iliyopo jamii ya Pwani kusini mwa jimbo la San Francisco nchini Marekani.

Taarifa ya Mkuu wa Kaunti ya eneo hilo, imesema imemhoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wasimamizi wa Kaunti ya San Mateo, Dave Pine ambaye amesema, mshukiwa Zhao Chunli (67), alikuwa ni mfanyakazi mwenye hasira.

Inasadikika kuwa mshukiwa wa mauaji, Zhao Chunli (67), alikuwa ni mfanyakazi mwenye hasira. Picha ya RNZ.

Amesema, watu wanne wameuawa katika shamba hilo na wengine watatu katika kampuni ya lori nje kidogo ya Half Moon Bay, mji ulio umbali wa maili 30 kusini mwa San Francisco, katika jimbo la California.

Matukio hayo yanakuja ikiwa ni siku mbili baada ya vifo vya watu 11 siku ya Jumamosi ya Januari 21, 2023 kwenye ukumbi wa densi baada ya sherehe za Luna zilizokuwa zikifanyika katika jimbo hilo la California.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 25, 2023
Odinga awataka Wakenya kususia ulipaji kodi