Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana, Ezekia Wenje, Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Simiyu, Gimbi Masaba (Chadema) na mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Sitta Tuma wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kupinduka.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la Magereza lililoko nje kidogo ya Mji wa Bariadi, wakati wakitoka Mwanza kuelekea Bariadi kwa ajili ya msafara.

Akizungumzia ajali hiyo, Tuma alieleza kuwa wote wako salama ingawa gari lililopinduka limeharibika vibaya hasa upande wa mbele.

“Tunamshukuru Mungu kwa uwezo na mapenzi yake ametuokoa, ilikuwa ajali mbaya na imetokea tunaiona. Gari liliharibika mbele, lakini sisi Mungu ametunusuru,” Tuma alisema.

Kwa upande wa Wenje, aliizungumzia ajali hiyo kuwa ilikuwa mbaya na kwamba kilichosaidia zaidi ni kutokuwepo kwa gari, pikipiki au mwendesha baiskeli katika eneo hilo wakati huo.

Chanzo: Mwananchi

Picha: Diamond apata mapokezi ya kitemi Kenya
BEN POL NA JUX WAPEANA MAKAVU KWENYE 'NAKUCHANA', usikilize hapa