Polisi nchini Kenya, imesema takriban watu 11, wakiwemo maafisa wanane wa polisi na chifu mmoja wa eneo hilo, wameuawa na wezi wa ng’ombe waliokuwa wakiwafukuza katika maeneo yenye ukame la Kaunti ya Turkana iliyopo kaskazini mwa nchi hiyo.
Wizi wa ng’ombe au migogoro kuhusu vyanzo vya maji au ardhi ya malisho ni jambo la kawaida katika maeneo ya wafugaji kaskazini mwa Kenya, ambayo inapakana na Ethiopia na Sudan Kusini.
Katika andiko la Polisi wa Kenya, kwenye ukurasa wao wa Twitter limesema, “uvamizi wa uhalifu na woga wa wezi wa mifugo dhidi ya umma na maafisa wa polisi” katika Kaunti ya Turkana, ambao walisema ulisababisha vifo vya watu 11: maafisa 8 wa polisi, raia 2 na chifu wa eneo hilo.
Maafisa wa polisi waliouawa walikuwa wakiwasaka watu wa kabila la Pokot ambao walikuwa wamevamia kijiji, kuiba na kukimbia na ng’ombe, na inaarifiwa kuwa, Novemba 2012, maafisa wa polisi 42 waliuawa katika shambulio la kuvizia ambalo halijawahi kushuhudiwa kaskazini mwa eneo la Baragoi.
Agosti 2019, pia katika eneo hilo la kaskazini, watu wasiopungua 12 waliuawa na wezi wa mifugo wanaoshukiwa kuwa Waethiopia wa kabila la Borana, katika eneo hilo lililokabiliwa na misimu minne mfululizo ya uhaba wa mvua iliyosababisha hali ya ukame tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980.
Kenya, nchi yenye nguvu kubwa ya kiuchumi katika Afrika Mashariki, inakabiliwa na ukame wa hali ya juu kwa miaka 40 sasa, huku njaa ikiathiri watu milioni 4 kati ya zaidi ya watu milioni 50 ambapo mito na visima vimekauka na uwepo wa uhaba wa malisho iuliosababisha vifo vya zaidi ya mifugo milioni 1.5.