Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, limesema tayari limeanza utekekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango la kuchukua hatua dhidi ya Askari Polisi waliotajwa kushirikiana na wanachi, kuharibu miundombinu ya Reli (SGR).
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeti Magomi wakati akizungumza na Dar24 Media na kueleza kuwa amepokea maelekezo na anaenda kwenye utekelezaji kwa haraka.
Aidha, ameeleza kutofurahishwa na baadhi ya watendaji wa jeshi la Polisi kujihusisha katika uhalifu badala ya kudhibiti uhalifu kwa jamii.
”Jeshi la Polisi tunafundishwa na tunaelekezwa kufuata sheria na kanuni kwa maana ya kufuata standing orders, maana yake ule uadilifu na kutenda kwa weledi kwahiyo siwezi nikajisikia vizuri na ndio maana nimekwambia nimechukulia very negatively na kulifanyia kazi ipasavyo na kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinakomeshwa” amesema Magomi.
Kamanda Magomi pia ameelezea namna ambavyo amejipanga kuwadhibiti watu kama hao ambao wanalichafua Jeshi la Polisi kwa kutokufuata sheria na kanuni za Jeshi hilo.
”Nimejipanga maana ya kwamba kuchuka hatua za kinidamu, lakini baada ya kuchuka hatua, na ninakwenda kwenye weledi wa kufanya opereshion, kwa maana ya kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo hivi” amesema
”Tutafanya doroa za pamoja lakini pia kupata taarifa za wahalifuna wale wananchi wa pembezoni na wafanyakazi wa kule ndani ambao sio waadili ambao wananfanya vitendo hivyo” amesema Magomi