Will Smith ameonesha kuwa na nguvu mpya za kurudi kwenye game ya Hip Hop baada ya kufunika kwenye jukwaa la Latin Grammy zilizotolewa Las Vegas, Marekani.

Smith alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki baada ya kupanda jukwaa kuchana mashairi ya ubeti wa remix ya wimbo ‘Fiesta’ akiwa na kundi la Bomba Estero la Colombia.

Ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 10, Smith alipigiwa shangwe na mkewe Jada Pinkett na mwanae Trey waliokuwa upande wa mashabiki hivyo kuongeza Morali zaidi.

Will Smith yuko katika maandalizi ya mwisho ya kuachia album yake mpya na tayari ameshaandaa mzigo wa nyimbo 30 kusapoti kishindo cha ujio wake mpya.

“Ni nakisikia nia ya kuendelea kuisukuma bahasha ya michano. Naweza kwenda umbali gani!? Hadi ntakapogota miaka 70 au 80,” alisema.

Lowassa akwama Mwanza, Polisi wawazuia Chadema Kuuaga mwili wa Mawazo kuhofia kipindupindu
Magufuli azilipua taasisi zilizotumia mabilioni angani